Wachezaji Azam FC kwenye hesabu nzito

WACHEZAJI wa Azam FC, matajiri wa Dar wapo kwenye hesabu nzito kuelekea mechi zijazo za ushindani msimu wa 2025/26.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Florent Ibenge katika mchezo uliopita ilitoshana nguvu na Namungo FC ilikuwa Novemba 9,2025.

Baada ya dakika 90 ubaowa Uwanja wa Majaliwa ulisoma Namungo 1-1 Azam FC. Ni Azam FC walianza kupata bao la kuongoza dakika ya 13 kupitia kwa Idd Nado likawekwa usawa na Fabrince Ngoyi dakika ya 51.

Kwenye msimamo wa ligi, Azam FC ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 5 kibindoni Namungo FC nafasi ya 10 pointi 6 baada ya mechi 6.

Lusajo Mwaikenda nahodha wa Azam FC amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ushindani na wana ari ya juu kupata matokeo kwa mechi zijazo.

“Wachezaji tuna ari ya juu na tutajitolea kwa asilimia 100 ili kupata matokeo mazuri kwenye mechi zetu. Mashabiki tunaomba waendelee kuwa pamoja nasi,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.