Aziz Andambwile kwenye maisha mapya Yanga SC

KIUNGO Aziz Andambwile kwa sasa yupo katika maisha mapya ndani ya kikosi cha Yanga SC baada ya kupoteza namba kikosi cha kwanza.

Aziz zama za Romain Folz alikuwa akianza kikosi cha kwanza mara baada ya kocha huyo kufutwa kazi Oktoba 18,2025 nchini Malawi hajawa chaguo la kwanza kwa Kocha Mkuu, Pedro Goncalves ambaye yupo Jangwani kwa sasa.

Mchezo wa mwisho kuanza kikosi cha kwanza ilikuwa Oktoba 18,2025 walipocheza na Silvers Strikers katika mchezo huo Yanga SC ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 Ligi ya Mabingwa Afrika alikomba dakika 78 nafasi yake ilichukuliwa na Duke Abuya.

Kwa sasa katika mechi za ligi amekuwa akianzia benchi na mchezo uliopita alipewa dakika 5 dhidi ya KMC FC, Uwanja wa KMC Complex.

Rekodi zinaonyesha kuwa Aziz amecheza mechi 3 za ligi akikomba jumla ya dakika 130 msimu wa 2025/26.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.