Jonathan Sowah bao lake lazua utata Bongo, Nangu atajwa

JONATHAN Sowah mshambuliaji wa Simba SC bao lake alilofunga kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania limezua utata huku ikielezwa kuwa alikuwa kwenye mtego wa kuotea.

Sowah alifunga bao hilo Novemba 8,2025 Uwanja wa Meja Isahmuyo wakati ubao uliposoma JKT Tanzania 1-2 Simba SC.

Mabao matatu yalipatikana kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani, Edward Songo alianza kufunga kwa JKT Tanzania na mabao ya Simba SC yalifungwa na Wilson Nangu kwa pigo la kichwa na Sowah kwa shuti akitumia pasi Morice Abraham.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa anachotambua wamepata ushindi kwenye mchezo mgumu wakitumia silaha walizokuwa nazo na mbinu za benchi la ufundi.

“Tulijua utakuwa mchezo mgumu na ndio maana unaona mabao yamefungwa kwa mbinu za kishujaa na wachezji wetu. Unaona pasi zinapigwa ambazo zinapenya katikati ya mabeki yaani wanajiuliza tuupige ama tusiupige maana ni pasi ya hatari.

“Tumetumia silaha ambazo tulizichukua JKT Tanzania hapa unamzungumzia mlinda mlango Yakoub na beki Nangu hawa ni watu kwelikweli na tunamshukuru Mungu tumepata pointi tatu,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.