Huyu hapa atajwa kuwa kocha mpya Yanga SC

INAELEZWA kuwa Yanga SC tayari wamekubaliana kila kitu na kocha mpya, Romuald Rakotondrabe ili kuwa kocho mpya hapo.

Taarifa zinaeleza kuwa kocha huyo huenda akasaini kandarasi ya miaka miwili kwa ajili ya kufanya kazi katika kikosi hicho kinachowakilisha Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Inaelezwa kuwa upande mwingine Romain Folz raia wa Ufaransa atapewa barua ya kufutwa kazi muda wowote kuanzia sasa.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka Yanga SC kocha huyo mpya anatarajiwa kutua nchini na benchi lake lote la ufundi kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho.

Licha ya tetesi hizo bado Folz yupo Jangwani akiendelea na majukumu yake huku taarifa mpya ikitarajiwa kutolewa muda wowote mpango kazi ukijibu.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.