WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga la kimataifa katika hatua ya awali wanakibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Wiliete SC Jumamosi hii.
Yanga SC itaingia uwajani ikiwa na faida ya ushindi wa mabao 3-0 waliyopata katika mchezo wa ugenini mabao yakifungwa na Aziz Andambwile aliyefungua ukurasa katika anga la kimataifa, Edmund John na Prince Dube.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC ameweka wazi kuwa mwisho wa mchezo wa ugenini ni mwanzo wa maandalizi kuelekea katika mchezo ujao wa kimataifa hivyo wapo tayari.
“Ushindi wetu ugenini haina maana kwamba kazi imekwisha bado tutaendelea kufanya maandalizi na malengo ni kuona kwamba tunavuka hii hatua tupo tayari na mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi.”
Yanga SC imetoka kucheza mchezo wa ufunguzi wa ligi dhidi ya Pamba Jiji ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 Septemba 24 2025, Septemba 27 2025 itakuwa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.