WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga la kimataifa, Yanga SC wamefungua pazia kwa ushindi mchezo wa hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Wiliete SC 0-3 Yanga SC mchezo huo ulichezwa Septemba 19 2025. Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Romain Folz inaanza kete yake ya kwanza kimataifa msimu wa 2025/26 kwa ushindi ugenini.
Magoli yamefungwa na Aziz Andambilwe dakika ya 31, Edmund John dakika ya 71 na Prince Dube dakika ya 79. Katika magoli hayo ni Edmund hakuanza kikosi cha kwanza alikuwa benchi na aliingia kipindi cha pili.
Yanga SC imepata ushindi huo ikiwa imetoka kupata ushindi kwenye mchezo dhidi ya Simba SC ambao ulikuwa wa Ngao ya Jamii uliochezwa Septemba 16 2025 Uwanja wa Mkapa kwa bao 1-0 ambalo lilifungwa na kiungo mshambuliaji Pacome.
Karata ya Yanga SC kimatafa ilichezwa Uwanja wa 11 de Novembro.Mchezo wa marudiano kwa wababe hawa unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Bakari Mwamnyeto nahodha wa Yanga SC amesema kuwa walikuwa na uchovu hasa baada ya kutoka kwenye mchezo mgumu wa Dabi lakini walituliza akili na kutumia nafasi ambazo walizipata.
“Tulitoka kwenye mchezo mgumu lakini tulikuwa makini na tulituliza akili kwenye mchezo wetu wa kimataifa. Tunamshukuru Mungu tumepata matokeo na tunawashukuru mashabiki kwa dua.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.