Yanga SC yakwea pipa baada ya kumalizana na Simba SC

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC, Yanga SC chini ya Kocha Mkuu Romain Folz wamekwea pipa kuelekea Angola kwa mechi ya kimataifa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Septemba 16 2025 saa 11:00 jioni, Yanga SC walikuwa na kazi kutetea taji la Ngao ya Jamii katika mchezo wa fainali dhidi ya Simba SC wakafanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 baada ya dakika 90.

Kwenye mchezo huo dakika 45 ngoma ilikuwa ngumu kwa timu zote kipindi cha pili upepo ulibadilika kwa Yanga SC kupata bao dakika ya 53 kupitia kwa Pacome ambaye alimtungua kipa namba moja Moussa Camara.

Mapema alfajiri ya Septemba 17 2025 kikosi cha Yanga SC kimekweka pipa kuelekea Angola kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo wa kimataifa ikiwa ugenini.

Timu hizo zitavaana katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa Ijumaa Septemba 19 Uwanja wa Estádio 11 de Novembro, Luanda Angola.

Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara ni Dickson Job, Israel Mwenda, Pacome, Djigui Diarra, Aziz Andambwile.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.