YANGA SC vs Simba SC wababe hawa wawili wanatarajiwa kuwa kwenye kazi ya kusaka ushindi ndani ya Uwanja Septemba 16 2025.
Zimebaki siku tatu kwa watani hawa wa jadi kupambania taji la Ngao ya Jamii ikiwa ni mchezo rasmi wa ufunguzi wa msimu mpya wa 2025/26.
Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 taji la Ngao ya Jamii lilichukuliwa na Yanga SC iliyopata ushindi kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Mkapa.
Simba SC iliondolewa na Yanga SC katika hatua ya nusu fainali kwa kufungwa bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Maxi Nzengeli alimtungua kipa namba moja Moussa Camara ambaye yupo kwenye kikosi cha Simba SC kuelekea msimu wa 2025/26.
Timu zote mbili zimetoka kupata ushindi kwenye mechi zao zilizopita za kimataifa ambazo zilikuwa ni za kirafiki.
Simba SC 2-0 Gor Mahia kwenye kilele cha Simba Day, Septemba 10 2025 na Yanga SC 1-0 Bandari kwenye kilele cha Yanga Day, Septemba 13 timu zote zilicheza Uwanja wa Mkapa.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.