INATAJWA kuwa baada ya kipa namba mbili wa Simba SC kukutana na Than You Septemba 5 2025 kuna uwezekano akaibukia ndani ya Fountain Gate.
Ni Ally Salim ambaye kwa msimu wa 2024/25 alikuwa chaguo la pili kikosi cha Simba SC na namba moja alikuwa ni Moussa Camara.
Chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids, Salim alianza kikosi cha kwanza kwenye mechi mbili za ligi akikomba dakika 180 na kwenye mechi hizo hakufungwa.
Itakumbukwa kwamba kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali Kombe la CRDB Federation Cup alianzia benchi na alipoingia alifungwa mabao mawili dhidi ya Singida Black Stars ambayo ilicheza fainali na watani wa jadi wa Simba SC, Yanga SC.
Inaelezwa kuwa Fountain Gate inafanya maboresho ya kikosi hicho huenda ikamsajili Ally Salim akiwa ni mchezaji huru.
Ally Salim hakuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa kambini nchini Misri ameagwa rasmi Septemba 5 2025 na Simba SC ambayo inatarajia kufanya tamasha la Simba Day, Septemba 10 2025, Uwanja wa Mkapa.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.