WAKATI kikosi cha Simba SC kikitarajiwa kurejea Tanzania leo Agosti 28 2025 inaelezwa kuwa tayari benchi la ufundi lina jina la mrithi wa mikoba ya Mohamed Hussen Zimbwe Jr ambaye alikuwa nahodha mkuu msimu wa 2024/25.
Zimbwe Jr kwa sasa hatakuwa ndani ya Simba SC msimu wa 2025/26 baada ya kupata changamoto mpya ndani ya Yanga SC. Inaelezwa kuwa benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids limechagua jina la Chamou Karabou kuwa nahodha.
Chamou Karabou ni beki anatarajiwa kuwa nahodha wa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids, rai awa Afrika Kusini. Msimu wa 2024/25 hakuwa chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Simba SC.
Rekodi zinaonyesha kuwa Chamou alicheza jumla ya mechi 19 za ligi akikomba dakika 1,480 ni alitoa pasi moja ya goli ndani ya ligi kati ya mabao 69 yaliyofungwa na Simba SC baada ya mechi 30.
Inaelezwa Fadlu anamuandaa Chamou kuwa mrithi wa aliyekuwa beki wa kushoto wa timu hiyo msimu wa 2024/25, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ awe nahodha msimu ujao.
Beki mkongwe wa kulia, Shomari Kapombe ambaye alikuwa nahodha namba tatu katika kikosi hicho, yeye atakuwa wa pili na siyo wa tatu kama ilivyokuwa msimu uliopita.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.