MAXIMO NA HESABU KUBWA NDANI YA KMC, MASHINE MPYA YATAMBULISHWA

MARCIO Maximo, Kocha Mkuu wa KMC ameweka wazi kuwa wanatambua namna ushindani ulivyo ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC hivyo muda wa maandalizi watatengeneza kikosi chenye ushindani.

Timu hiyo yenye maskani yake Kinondoni inatumia Uwanja wa KMC Complex kwa mechi za nyumbani tayari ipo kambini Zanzibar kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26.

Rasmi leo Agosti 7 2025 KMC imemtambulisha mchezaji mpya ambaye atakuwa chini ya benchi la ufundi la Maxime ambaye alikuwa ndani ya Mashujaa msimu wa 2024/25 anaitwa  Ibrahim Nindi .

Ibrahim alikuwa sehemu ya kikosi cha Mashujaa msimu uliopita, alikuwa sehemu kikosi cha Timu ya Taifa ya Ngorongoro Heroes ambacho kilishiriki mashindano ya AFCON nchini Misri.

Kocha amesema: “Tunatambua ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji kupata matokeo mazuri. Tuna amini kwa ushirikiano wetu tutafanya kazi kubwa kutafuta matokeo kwenye mechi zetu ambazo tutacheza. Tunawaomba mashabiki mjitokeze kwa wingi kwenye mechi zetu ambazo tutacheza tukiwa nyumbani na ugenini.”

Ligi Kuu Tanzania Bara msimu mpya wa 2025/26 unatarajiwa kuanza kurindima Septemba 16 2025 kwa kila timu kushuka uwanjani kusaka ushindi.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.