SIMBA SC chini ya Kocha Mkuu Fadlu Davids wanaendelea na matizi ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26.
Katika kambi iliyopo Misri wachezaji wapya na wale waliokuwa katika kikosi cha Simba SC iliyogotea nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wapo kambini.
Miongoni mwa wachezaji waliopo ndani ya kikosi cha Simba SC ni Kibu Dennis ambaye huyu alikuwa nchini Marekani wakati wa likizo huku Moussa Camara ambaye ni kipa namba moja naye akiwa yupo kwenye orodha ya wachezaji waliopo katika kikosi.
Camara ni kipa namba moja kwa kukusanya hati safi msimu wa 2024/25 alipokusanya jumla ya hati safi 19 ndani ya ligi ya NBC ambayo ni namba nne kwa ubora.
Mbali na Kibu Dennis yupo Mzamiru Yassin kiungo wa kazi ngumu ambaye msimu wa 2024/25 hakuwa fiti kwa asilimia 100 kwenye mechi za ushindani.
Leonel Ateba na Steven Mukwala ambao ni washambuliaji nao wapo kambini kwa maandalizi ya msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Miongoni mwa wachezaji wapya waliopo kambini ni nyota aliyetambulishwa Agosti 2 2025 Simba SC ambaye ni Mohamed Bajaber. Kiungo mshambuliaji alikuwa anacheza Polisi ya Kenya.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.