HIKI HAPA CHUMA CHA PILI KUTAMBULISHWA SIMBA SC

Baada ya Rushine De Reuck Julai 29 akiwa ni beki na mchezaji wa kwanza kutambulishwa unyamani, Julai 30 nyota mwingine ametambulishwa.

Ni Alassane Kante ambaye ni kiungo aliyekuwa anacheza CA Bizertin ya Tunisia atakuwa ndani ya Simba SC msimj wa 2025/26.

Kante aliwaaga mashabiki wake Tunisia na video yake ilizua gumzo wakati akiwaaga mashabiki wa Bizertin ambapo wapo mashabiki waliokuwa wakionekana kulia.

Nyota huyo anakuwa ni mchezaji wa pili kutambulishwa Simba SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Kikosi cha Simba SC kimekwea pipa kueleka Misri kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26.

Tayari kikosi kipo Ismailia kwa kuanza maandalizi ya msimu mpya. Miongoni mwa wachezaji waliopo kambini ni mchezaji mpya Rushine, Leonel Ateba, Joshua Mutale na Jean Ahoua.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.