MSHAMBULIAJI bora wa muda wote kwa sasa raia wa Ureno Cristiano Ronaldo ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha Diogo Jota na kaka yake Andre Silva.
Ulimwengu wa mpira kwa sasa unaomboleza kufuatia kutangulia mbele za haki kwa kijana huyo mwenye miaka 28. Kijana huyo alikuwa kwenye safari kuelekea kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26 ndani ya Klabu ya Liverpool.
Ronaldo ameonesha masikitiko yake akisema ni hivi majuzi tu walikuwa wote kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ureno lakini pia ni juzi tu Jota ameoa hii inakuwa ngumu kuipokea kuwa leo amefariki.
Nahodha huyo wa Ureno ametuma salamu za pole kwa familia ya Jota na wapenda soka ulimwenguni kwa msiba huo mzito wa Jota na Adre.