MILOUD Hamdi, Kocha Mkuu wa Yanga SC amesema kuwa furaha kubwa ni kuona timu hiyo inaendelea kupata matokeo mazuri na kutwaa mataji ambayo walikuwa wanayatafuta.
Kwenye fainali ya CRDB Federation Cup, Juni 29 2025 Yanga SC ilishinda mabao 2-0 dhidi yaSingida Black Stars fainali iliyopigwa Uwanja wa New Amaan Complex. Mabao ya Duke Abuya dakika ya 39 na Clement Mzize dakika ya 49 yalitosha kuwapa ubingwa mabingwa hao watetezi.
Miloud amesema: “Kikubwa ni kuona malengo yetu tunayafikia na ilikuwa hivyo tangu mwanzo wa msimu. Wachezaji wanatimiza majukumu kwa umakini na hili ni jambo kubwa kila wakati wanastahili pongezi.
“Wachezaji wanacheza kwa juhudi kubwa na kupata matokeo hili ni kubwa. Uongozi wa Yanga SC umekuwa nasi bega kwa bega katika hili nalo wanastahili pongezi kwa kuwa kazi hii sio nyepesi.”
Yanga SC inakuwa imetwaa mataji matano msimu wa 2024/25 ilianza na Toyota Cup, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara, Kombe la Muungano na CRDB Federation Cup.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.