CHINI ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids, Simba SC imekwama kuvuna pointi mbele ya Yanga SC ambao ni watani zao wa jadi.
Matukio mawili yamekamilisha msimu wa 2024/25, ubingwa kwa Yanga SC wakiwa na pointi 82, Simba SC nafasi ya pili na pointi 78.
Katika dakika 180, mbele ya Yanga SC, Moussa Camara kipa namba moja wa Simba SC ametunguliwa mabao matatu na Simba SC imepoteza pointi sita mazima na kupishana na ubingwa.
Mzunguko wa kwanza ilikuwa Simba SC 0-1 Yanga SC na mzunguko wa pili ilikuwa ni Yanga SC 2-0 Simba SC.
Fadlu ameweka wazi kuwa walikuwa wanahitaji matokeo ili kupata ubingwa mwisho wamepishana nao na kuwapa pongezi Yanga SC kwa kutwaa ubingwa.
“Pongezi kwa Yanga SC kwa kutwaa ubingwa , mchezo wetu ulikuwa na ushindani mkubwa mwisho makosa ambayo tumefanya yametugharimu. Tulikuwa na msimu mzuri kwa kuwa tumefikia malengo kwa kiasi kikubwa.
“Kuna namna ambayo tunapaswa kufanya kazi kubwa hasa kwenye eneo la wachezaji kuwa kwenye ubora katika mechi kubwa, tunao wanafanya vizuri na wanastahili pongezi.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.