MOUSSA Camara kipa namba moja wa Simba SC ameifikia rekodi ya Aishi Manula kipa wa Simba SC katika kukusanya hati safi ndani ya uwanja kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.
Camara, Juni 22 2025 alianza kikosi cha kwanza dhidi ya Kagera Sugar na aliokoa hatari mbili zilizokuwa zinakwenda langoni mwake ya kwanza ilikuwa dakika ya 24 ni Momo wa Kagera Sugar jaribio lake akiwa ndani ya 18 liliokolewa.
Dakika ya 42 Mahundi alifanya jaribio ambalo liligotea kwenye mikono ya Camara ambaye alipiga shuti lililolenga lango na mwisho ubao wa Uwanja wa KMC Complex ukasoma Simba SC 1-0 Kagera Sugar bao la Steven Mukwala dakika ya 17.
Ni hati safi 19 anafikisha Camara akiwa anaongoza katike eneo hilo huku anayemfuatia akiwa ni Djigui Diarra wa Yanga mwenye hati safi 16 msimu wa 2014/25.
Camara ameifikia rekodi ya Aishi Manula ambayo aliiandika msimu wa 2017/18 alipokuwa kipa namba moja wa Simba SC kwa msimu wa 2024/25 Air Manula hajakaa langoni mchezo hata mmoja wa ligi.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.