MSHAMBULIAJI WA MABAO MLANGONI YANGA SC

JONATHAN Sowah mshambuliaji wa Singida Black Stars anatajwa kuwa kwenye mpango wa kutakiwa na Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.

Sowah alimpa tabu kipa namba moja wa Yanga SC, Djigui Diarra kwenye mchezo wa ligi walipokutana Uwanja wa KMC Complex kwa kumtungua bao moja.

Kwenye mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga SC 2-1 Singida Black Stars, Sowah alifunga bao lakufutia machozi mbele ya vinara wa ligi.

Taarifa zinaeleza kuwa mchezaji mwenyewe anapenda kucheza ndani ya kikosi cha Yanga SC jambo ambalo linatoa nafasi kubwa kwa mabingwa watetezi kuipata saini yake.

Mshambuliaji huyo anayevaa jezi namba 3 ndani ya ligi amefunga jumla ya mabao 11 akiwa ni miongoni mwa washambuliaji wenye mabao mengi licha ya kujiunga na timu hiyo kwenye dirisha dogo la usajili.

Singida Black Stars ni nafasi ya nne kwenye msimamo ina pointi 53 safu ya ushambuliaji imefunga mabao 40 baada ya mechi 28 mchezo wao ujao ni dhidi ya Dodoma Jiji unatarajiwa kuchezwa Juni 18 2025 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.