MABINGWA watetezi wa CRDB Federation Cup, Yanga SC wamebainisha kuwa mpango mkubwa ni kutwaa taji hilo kwa mara nyingine kutokana na uimara wa kikosi walichonacho.
Yanga SC imeandika rekodi ya kutinga fainali ya CRDB Federation Cup mara tano ikiwa ni timu ambayo imekuwa kwenye mwendelezo mzuri katika kuandika rekodi kali ambazo bado hazijavunjwa.
Ipo wazi kwamba ndani ya Ligi Kuu Bara inashikilia rekodi ya kucheza jumla ya mechi 49 bila kupoteza na ilipoteza mchezo wake dhidi ya Ihefu kwa kufungwa mabao 2-1 wakati ikisaka rekodi yakufia jumla ya mechi 50 bila kufungwa.
Ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania unaipa tiketi Yanga SC kutinga hatua ya fainali ambapo inamsubiri mshindi wa mchezo kati ya Simba SC vs Singida Black Stars unaotarajiwa kuchezwa Mei 31, 2025.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema kuwa mpango mkubwa ni kupata ushindi kwenye mechi zilizobaki ili kutwaa mataji ambayo wanatetea.
“Kwenye CRDB Federation Cup tunaamini kwamba ushindani ni mkubwa baada ya kufika fainali hesabu ni kupata matokeo kwenye mchezo wetu unaofuata ambao ni wa hatua ya fainali.”
Kuingia fainali mara tano mfululizo kunaifanya Yanga SC kushinda jumla ya mechi 23 bila kupoteza kwenye mashindano haya ambapo ili rekodi ivunjwe na timu nyingine ni lazima iingie fainali mara nne mfululizo.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.