Jean Ahoua kwenye mtihani mzito ugenini kimataifa dhidi ya RS Berkane Mei 17 2025.
Ligi Kuu Bara anaongoza kwa kufunga mabao mengi akiwa nayo 15 kibindoni.
Ahmed Ally Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC abainisha bado sana.
KIUNGO mshambuliaji wa Simba SC, Jean Ahoua ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids ana kazi kubwa kwenye mchezo wa leo Mei 17 2o25 ambao ni hatua ya fainali ya kwanza dhidi ya RS Berkane kutokana na wababe wote hawa wawili kulitaka kombe la Shirikisho Afrika.
Ndani ya ligi, Ahoua amecheza jumla ya mechi 24 kati ya 26 ambazo zimechezwa na Simba SC akifunga mabao 15 na kutoa pasi 7 za mabao akihusika kwenye mabao 22 kati ya 62 yaliyofungwa na Simba SC.
Rekodi zinaonyesha kuwa kwenye mabao 15 ambayo kafunga, mabao 14 katupia kwa mguu wa kulia huku bao moja akifunga kwa pigo la kichwa ilikuwa mchezo dhidi ya Pamba Jiji alipotumia pasi ya Ellie Mpanzu Uwanja wa KMC Complex.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa bado kiungo Ahoua hajafikia asilimia 100 ya ubora wake licha ya kazi anayofanya uwanjani.
“Yule Ahoua bado hajafikia asilimia 100 ya uwezo wake kwani kocha anatengeneza kikosi nasi tupo kwenye hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika ambacho tunahitaji ni kuona kwamba kila mchezaji anakuwa kwenye ubora mkubwa.
“Ni kama asilimia 32 ambazo anazo kwa sasa ni hizo chache zinafanya kazi hivyo kikosi kikifikia asilimia 100 watu watasusa vibaya mno kukutana na Simba SC.
“Tunawaheshimu wapinzani wetu RS Berkane lakini lazima watambue kwamba sisi tunahitaji ushindi kwenye mchezo wetu tutapambana kwa kuwa tupo tayari kwa kupata matokeo mazuri.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.