LIGI KUU BARA RATIBA HII HAPA MEI 12 2025

MEI 12 2025 Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo ikiwa ni mzunguko wa pili kwa wababe kuwa uwanjani kusaka pointi tatu muhimu.

Tanzania Prisons ambayo ipo nafasi ya 14 kwenye msimamo na pointi 27 baada ya kucheza mechi 27 itawakaribisha Coastal Union ya Tanga ambayo ipo nafasi ya 8.

Coastal Union imecheza mechi 27 na kukusanya jumla ya alama 31 sawa na Namungo FC ambayo ipo nafasi ya 9 kwenye msimamo huku Coastal Union ikiwa nafasi ya 8.

Kagera Sugar ambayo ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 22 itawakaribisha Mashujaa FC iliyo nafasi ya 10 kwenye msimamo na pointi 30 katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Kaitaba.

Ikumbukwe kwamba vinara wa ligi ni Yanga SC wenye pointi 70 baada ya kucheza mechi 26 wanafuatiwa na Simba SC nafasi ya pili na pointi 69.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.