MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi wapo kwenye maandalizi kuelekea mchezo wa mzunguko wa pili dhidi ya Namungo FC unaotarajiwa kuchezwa Mei 13 2025.
Yanga SC ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 70 baada ya kucheza mechi 26 ni ushindi kwenye mechi 23 wakiambulia sare mchezo mmoja dhidi ya JKT Tanzania na kupoteza mechi mbili.
Wanakutana na Namungo FC iliyo nafasi ya 9 kwenye msimamo na pointi 31 baada ya kucheza jumla ya mechi 27 ikiwa imepata ushindi kwenye mechi 8, sare 7 ikipoteza mechi 12.
Miloud ameweka wazi kuwa mechi zote ambazo wanacheza ndani ya uwanja ni muhimu kupata pointi tatu kutokana na malengo ambayo wanayo kwenye mechi zote wanazocheza ndani ya uwanja.
“Kikubwa ambacho tunahitaji kwenye mechi zetu ni pointi tatu hilo lipo wazi, maandalizi mazuri yanatupa nguvu ya kupata matokeo chanya hivyo tupo tayari kwa mechi zetu na ukiwa Yanga SC ni lazima ukubali kujitoa kupata pointi.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.