Klabu ya Simba imemualika mkuu wa mkoa wa Tabora, Paul Matiko Chacha kujumuika na WA Tanzania wengine kushuhudia mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) dhidi ya Al Masry katika dimba la Benjamin Mkapa Aprili 9, 2025.
Akizungumza kwenye hamasa za mashabiki kuelekea mchezo huo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Sc, Ahmed Ally amebainisha sababu za kumualika Mhe. Chacha ni mchango wake wa kuhamasiha michezo na ajifunze namna maandalizi ya kimataifa yanafanyika kwa ajili ya kuiandaa timu yake ya Tabora United.
“Tunamualika Mkuu wa Mkoa wa Tabora aje ashuhudie namna Mashindano makubwa yanavyochezwa maana na yeye anayo timu nzuri ambayo haipo kwenye nafasi mbaya hivyo tunamualika kwenye mchezo wetu, Adui yao sisi ndio rafiki yetu” — amesema Ahmed Ally