NASSORO Saadun amefikisha mabao sita ndani ya Azam FC baada ya kupachika bao moja mbele ya Ken Gold dakika ya 39 kwa mguu wa kushoto akitumia pasi ya Pascal Msindo.
Kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa kazi ilimalizika dakika 45 za kipindi cha kwanza, Mbeya.
Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Ken Gold 0-2 Azam FC, safu ya ushambuliaji ya Azam FC inafikisha jumla ya mabao 38 kwa msimu wa 2024/25 na vinara kwenye kufunga mabao mengi ni Yanga wenye mabao 61.
Kazi ilianza dakika ya 27 kwa Gibril Sillah akiwa ndani ya 18 kupachika bao kwa mguu wa kushoto akitumia pasi ya Idd Nado ambaye alimpa kwa mguu wa kulia akiwa ndani ya 18 ilikuwa ni Aprili 3 2025.
Sillah alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo wakiwa ugenini baada ya dakika 90 kugota mwisho.
Azam FC inafikisha pointi 51 ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 24, Ken Gold nafasi ya 16 pointi 16 baada ya mechi 24 ipo kwenye mstari wa kushuka daraja.
Timu mbili baada ya mzunguko wa pili kugota mwisho zitashuka daraja moja kwa moja ni zile zitakazokuwa nafasi ya 16 na 15 ambapo kwa sasa nafasi ya 15 ipo mikononi mwa Tanzania Prisons yenye pointi 18 baada ya mechi 24.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.