WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga la kimataifa Simba katika Kombe la Shirikisho Afrika wameweka wazi kuwa hesabu kubwa ni kupata ushindi kwenye mchezo wa pili wa robo fainali dhidi ya Al Masry unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Ipo wazi kuwa kwenye mchezo wa robo fainali ya kwanza iliyochezwa Aprili 2 2025 Uwanja wa Suez Canal baada ya dakika 90 ubao ulisoma Al Masry 2-0 Simba ukiwa ni mchezo wa kwanza kimataifa Simba kuyeyusha dakika 90 bila kufunga bao.
Mabao kwenye mchezo huo yalifungwa kila moja kipindi chake, ambapo kipindi cha kwanza ni Abderrarhim Deghmoum alianza kupachika bao la uongozi dakika ya 15 kwa shuti kali akiwa nje ya 18 likimshinda Moussa Camara.
Kipindi cha pili ilipachikwa kamba ya pili ambayo ni mali ya John Okoyo dakika ya 89. Mfungaji wa bao la pili alianzia benchi kwenye mchezo huo alipoingia alipachika bao hilo akiwa ndani ya 18.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua matokeo ambayo wameyapata sio mazuri kutokana na ushindani ulivyo ila wana nafasi kufanya vizuri kwenye mchezo wao ujao Uwanja wa Mkapa.
“Hayakuwa matokeo mazuri kwetu ipo wazi kwani wachezaji wetu walipambana kusaka ushindi na mwisho tumepoteza, nguvu kubwa sasa ni kuelekea mchezo wetu wa nyumbani Uwanja wa Mkapa, hakika hi tunavuka.”
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 9 2025 Uwanja wa Mkapa na mshindi wa mwisho katika mchezo huo atatinga hatua ya nusu fainali ili Simba apenye ni lazima afunge mabao zaidi ya mawili.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.