WANANCHI WATOA KIKOSI KUMKABILI MNYAMA

WANANCHI Yanga licha ya taarifa kueleza kuwa hakutakuwa na mchezo  dhidi ya Simba, Uwanja wa Mkapa Machi 8 2025 wamefika uwanjani na kutoa kikosi kazi kitakachoikabili Simba kusaka pointi tatu muhimu.

Kwenye kikosi hicho Aziz Ki ameanzia benchi na kiungo Clatous Chama huku ingizo jipya Ikangalombo naye akiwa benchi.

Kikosi chenyewe kipo namna hii:-

Djigui Diarra, Israel Mwenda, Boka, Dickson Job, Bacca, Aucho, Maxi Nzengeli, Duke Abuya, Prince Dube, Pacome na Mzize hawa wanatarajiwa kuanza kikosi cha kwanza.

Wachezaji wa akiba ni Mshery, Nondo, SureBoy, Wilson, Mudathir, Shekhan, Ikangalombo, Aziz Ki, Clatous Chama. Ikumbukwe kwamba mchezo huu utapangiwa tarehe na Bodi ya Ligi.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.