GOD IS GOD, YANGA YATEMBEZA 5 G

MUNGU ni mwema kila wakati ni ujumbe wa kiungo mshambuliaji wa Yanga Maxi Nzengeli ambaye alikuwa nje kwa muda kutokana na kutokuwa fiti na amerejea uwanjani Januari 25 2025 akitupia bao moja dhidi ya Copco FC raundi ya tatu CRDB Federation Cup.

Baada ya dakika 90 Ubao wa Uwanja wa KMC, Complex umesoma Yanga 5-0 Copco ambapo mabao yamefungwa na Shekhan Khamis dakika ya 35 akitumia pasi ya Farid Mussa, Prince Dube dakika ya 57 huyu alitumia pasi ya Israel Mwenda.

Maxi amepachika bao la tatu kwa mkwaju wa penalti baada ya nahidha wa Copco kumchezea faulo Maxi ndani ya 18, baada ya kufunga bao hilo Maxi alishangilia na kuonysha ujumbe unaosomeka God is God.

Mabao mengine yamefungwa na Duke Abuya dakika ya 77 na Mudathir Yahya kamba ya tano amepachika dakika ya 84.

Kesho Januari 26 2025 ni Simba v Kilimanjaro Wonders saa 10:00 jioni.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.