Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS) limeitangaza Ligi Kuu ya Tanzania (NBC Premier League) kuwa Ligi ya nne (4) kwa ubora barani Afrika na ya 57 duniani kwa mwaka 2024.
Ligi hiyo imepanda kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya sita mwaka 2023 ikizipiku Ligi za Afrika Kusini na Tunisia ikiwa nyuma ya vinara Ligi kuu Misri, Morocco iliyopo nafasi ya pili na Algeria ambayo ipo nafasi ya tatu huku Tunisia ikikamilisha tano bora kwa Afrika.
1. 🇪🇬 Nile Premier League — Egypt
2. 🇲🇦 Botola Pro League — Morocco
3. 🇩🇿 Ligue 1 — Algeria 🇩🇿
4. 🇹🇿 NBC Premier League — Tanzania
5. 🇹🇳 Ligue 1 Pro — Tunisia