BEKI wa Yanga, Dickson Job amesema kuwa furaha kubwa kupata ushindi dhidi ya Al Hilal inawekwa kando sasa nguvu kubwa ni kuelekea mchezo wao wa kimataifa dhidi ya MC Alger.
Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Sead Ramovic ipo nafasi ya tatu kwenye kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika ni pointi 7 imekusanya inatarajiwa kumenayana na MC Alger, Januari 18 2025.
Katika mchezo uliopita ugenini, Yana iliibuka na ushindi wa bao 1-0 likufungwa na Aziz Ki ambaye alitumia pasi ya Job ilikuwa dakika ya 7.
Tayari kikosi cha Yanga kimetua Dar kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo huo ambao umeshikilia tiketi ya Yanga kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Tumepata ushindi ugenini na kila mchezaji alikuwa anatambua kwamba kinachohitajika ni ushindi, nguvu yetu sasa ni kuelekea kwenye mchezo wetu wa nyumbani tunahitaji ushindi kufikia malengo ya kutinga hatua ya robo fainali.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.