BAADA ya MC Alger kupata ushindi dhidi ya TP Mazembe ubao uliposoma MC Alger 1-0 TP Mazembe, wamefikisha pointi 8.
Bao pekee la MC Alger lilifungwa na Akram Bouras dakika ya 36 kwa mkwaju wa penalti iliyoleta utata ilidumu mpaka mwisho wa mchezo.
Al Hilal nafasi ya kwanza pointi 10, MC Alger nafasi ya pili na Yanga ni pointi 4 nafasi ya tatu wakati TP Mazembe nafasi ya nne pointi mbili wakipoteza michezo mitatu.
Yanga kutoka Tanzania kete yao ya Januari 12 2025 dhidi ya Al Hilal wanazisaka pointi tatu kufikisha pointi 7 na fainali yao itakuwa Uwanja wa Mkapa dhidi ya MC Alger ambao wanasaka pointi tatu kutinga hatua ya robo fainali.
Kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sead Ramovic mchezo wake uliopita ilikuwa dhidi ya TP Mazembe ambapo walipata pointi tatu mazima kwa ushindi wa mabao 3-1.
Mabao ya Yanga yalifungwa na Clement Mzize aliyetupia mabao mawili na bao moja lilifungwa na Aziz Ki. Yanga inakibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Al Hilal Januari 12 2025 mchezo wa kuwania kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.