BEKI wa kupanda na kushuka Israel Mwenda ameanza mazoezi ikiwa ni maandalizi kwa mechi za ushindani msimu wa 2024/25 akiwa na uzi wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Sead Ramovic.
Mwenda ambaye ni beki ameibuka hapo akitokea kikosi cha Singida Black Stars alitambulishwa rasmi Desemba 11 2024 kuwa ni njano na kijani.
Amekutana na baadhi ya wachezaji ambao aliwahi kufanya nao kazi katika kikosi cha Simba ikiwa ni Mwamba wa Lusaka Clatous Chama, Jonas Mkude pia yupo Jean Baleke ndani ya Yanga hawa wote waliwahi kucheza ndani ya kikosi cha Simba.
Beki huyo akiwa na Singida Black Stars rekodi zinaonyesha kuwa alianza kikosi cha kwanza kwenye mechi tatu kati ya 12 ambazo timu hiyo ilishuka uwanjani ikikusanya pointi 24. Alipokuwa ndani ya Simba msimu wa 2023/24 alicheza jumla ya mechi 14 za ligi akikomba dakika 857.
Mwenda amesema ni furaha kwake kuwa kwenye changamoto mpya ndani ya kikosi cha Yanga kwa kuwa ni timu kubwa anaamini watafanya kazi kwa ushirikiano kupata matokeo mazuri.
“Ninafurahi kuwa hapa ndani ya Yanga kwa kuwa ni timu kubwa nina amini kwamba tutapata matokeo mazuri kwa ushirikiano.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.