YANGA YAIVUTIA KASI TP MAZEMBE

Meneja wa Yanga, Walter Harson amesema kuwa walianza maandalizi kuelekea mchezo wao dhidi ya TP Mazembe wakiwa Uarabuni, Algeria hivyo kwa sasa ni mwendelezo kuwa imara ili kupata matokeo kwenye mchezo ujao wa hatua ya makundi.

Katika mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga ilikwama kusepa na pointi tatu zaidi ya kugotea kuzipoteza hivyo ina kazi kusaka pointi tatu mbele ya TP Mazembe Desemba 14.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ilikuwa Yanga 0-2 Al Hilal na mchezo wa pili ugenini ilikuwa MC Alger 2-0 Yanga hivyo safu ya ulinzi imeruhusu mabao manne na safu ya ushambuliaji haijafunga bao kimataifa.

Tayari kikosi cha Yanga kipo Dar kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea kwenye mchezo wao ujao wa kimataifa ambao utakuwa ni watatu.

Harrison amesema: “Tunaendelea na maandalizi hapa nyumbani huu ni mwendelezo kwa kuwa tulianza maandalizi tangu Algeria baada ya mchezo wetu dhidi ya MC Alger. Kikubwa ni utayari na wachezaji wanaendelea vizuri kwa ajili ya kuona tunapata matokeo mazuri ugenini.”

Msafara wa mashabiki umeanza safari kuelekea Dr Congo na kikosi kinatarajiwa kukwea pipa Desemba 12 2024.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.