KOCHA Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic amesema kuwa matokeo ambayo wameyapata ugenini kimataifa walikuwa hawajatarajia hivyo watafanyia kazi makosa kuwa bora kwa mechi zijazo kitaifa na kimataifa.
Yanga haijaanza kwa mwendo mzuri kimataifa hatua ya makundi kwenye mechi mbili mfululizo ikipoteza pointi sita msimu wa 2024/25 kituo kinachofuata itakuwa ugenini dhidi ya TP Mazembe.
Ikumbukwe kwamba Desemba 8 2024, Al Hilal walikomba pointi tatu dhidi ya TP Mazembe kwa ushindi wa mabao 2-1 ambapo bao la ushindi kwa Al Hilal lilifungwa dakika ya 90 kupitia kwa Jean Cloude na bao la uongozi lilifungwa dakika ya 21 kwa mkwaju wa penalti kupitia kwa Mohamed Abdelrahman huku lile la TP Mazembe likifungwa dakika ya 64 na mtupiaji ni Oscar Kabwit.
Kundi A vinara ni Al Hilal wakiwa na pointi sita kibindoni wanafuatiwa na MC Alger wenye pointi nne, TP Mazembe ni pointi moja wakiwa nafasi ya tatu na kutoka Tanzania wawakilishi Yanga wapo nafasi ya nne wakiwa hawajakomba pointi baada ya kucheza mechi mbili ambazo ni dakika 180.
Desemba 14 itakuwa ni TP Mazembe v Yanga watakuwa ugenini kwa mara nyingine tena kimataifa baada ya kutoka ugenini na sasa wapo njiani kurejea Dar kwa ajili ya maandalizi mengine ya kuelekea DR Congo kwenye mchezo wao ujao kimataifa ugenini.
Desemba 19 itakuwa dhidi ya Mashujaa mchezo wa ligi unatarajiwa kuwa mchezo wa kwanza ndani ya Uwanja wa KMC, Complex. Desemba 22 2024 itakuwa ni Yanga v Tanzania Prisons huu pia ni NBC Premier League Uwanja wa KMC Complex.
Desemba 25 itakuwa ni dhidi ya Dodoma Jiji watakuwa ugenini na funga kazi ni Desemba 29 2024 dhidi ya Kagera Sugar, watakuwa nyumbani.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.