MASTAA HAWA WANNE YANGA HATIHATI KUIKOSA NAMUNGO

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga chini ya Kocha Mkuu, Sead Ramovic wanakibarua cha kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya Namungo huku nyota wanne wakitarajiwa kuukosa mchezo huo wa ligi.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majaliwa saa 12:30 kwa wababe wawili kuwa kwenye hesabu za kusaka pointi tatu muhimu baada ya dakika 90.

Miongoni mwa nyota ambao wanatarajiwa kutokuwa kwenye mchezo wa leo ni Ibrahimu Bacca ambaye ni beki huyu ana adhabu ya kadi nyekundu ya moja kwa moja aliipata kwenye mchezo dhidi ya Azam FC hakuwa kwenye kikosi mchezo dhidi ya Tabora United.

Mbali na Bacca kiungo Aziz Andambwile naye bado hajawa fiti kama ilivyo kwa Khalid Aucho na Clement Mzize ambao walipata maumivu wakiwa kwenye majukumu yao ya kazi.

Katika mchezo uliopita wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika mastaa hao hawakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga ambacho kilishuhudia ubao ukisoma Yanga 0-2 Al Hilal.

Leo Yanga itakuwa kwenye mchezo wa ligi ya Namungo ambapo Ramovic amebainisha kuwa wamefanyia kazi makosa yaliyopita kuwa bora zaidi.

“Tumekuwa na muda mzuri wa kufanya mazoezi pamoja kazi yetu ni kutafuta pointi tatu kwenye mchezo wetu dhidi ya Namungo na tunajua kwamba haitakuwa rahisi.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.