KWENYE mchezo dhidi ya Pamba Jiji Novemba 22 2024 nyota wa Simba, Jean Ahoua anaingia kwenye orodha ya wachezaji waliopoteza pasi nyingi katika dakika 45 ambazo alicheza.
Hajawa katika utulivu mchezaji wa matukio muhimu lakini katika ukabaji bado hajawa imara anapaswa kuongeza juhudi zaidi.
Miongoni mwa dakika ambazo alipoteza pasi ilikuwa dakika ya 15, 16, 30, 32, 33, 44.
Rekodi zinaonyesha huyu ni namba moja kwa utupiaji akiwa na mabao matano ndani ya kikosi cha Simba na pasi nne za mabao. Kahusika kwenye mabao 9 kati ya 22 yaliyofungwa na timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.
Simba ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kimataifa Afrika ambao ni wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Bravos ya Angola mchezo unaotarajiwa kuchewa Uwanja wa Mkapa, Novemba 27 2024 saa 10:00 jioni kwa wababe hao kuwa uwanjani kusaka pointi tatu muhimu ikiwa ni hatua ya makundi.
Ikumbukwe kwamba Yanga inawakilisha Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu dhidi ya Al Hilal ya Sudan saa 10:00 jioni Uwanja wa Mkapa.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.