TAIFA STARS KAZINI DHIDI YA GUINEA KWA MKAPA

FT: UWANJA: Mkapa

Kuwania Kufuzu AFCON 2025

Tanzania 1-0 Guinea

Goal Simon Msuva dakika ya 62

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayofundishwa na Hemed Morocco ina kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya timu ya taifa ya Guine kwenye mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2025 Uwanja wa Mkapa.

Nyota Simon Msuva ambaye alifunga bao kwenye mchezo uliopita dhidi ya Ethiopia amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini wapo tayari kwa ushindi.

Morocco amesema kuwa watafanya kazi kubwa kutafuta ushindi wakiwa nyumbani mbele ya mashabiki ambao wamejitokeza kwa wingi.