Kikosi cha ‘Stars’ kinachoanza dhidi ya Guinea kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi H wa kuwania kufuzu kombe la Mataifa Afrika AFCON 2025 katika dimba la Benjamin Mkapa.
Kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ amefanya badiliko moja kutoka kikosi kilichowanyoa Ethiopia huku kiungo Adolf Mtasingwa Bitegeko akichukua nafasi ya Novatus Dismans Miroshi ambaye anakosekana kwenye mchezo huo kutokana na msururu wa kadi za njano.