MEYA KUMBILAMOTO AUNGANA NA RAIS SAMIA KUWAPA POLE KARIAKOO

MEYA wa Jiji la Dar, Omary Kumbilamoto kwa  niaba ya Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar ametoa pole kwa Watanzania wote kutokana na tukio la kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo.

Ikumbukwe kwamba kwa sasa Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia vyombo vya usalama, Wananchi, Wafanyabiashara, Wanamichezo, mabondia wameungana kutokana na janga hilo ambalo lilitokea Novemba 16 2024.

Ajali hiyo ya kuporomoka kwa jengo la biashara lililopo mtaa wa Mchikichini Kariakoo ilitokea asubuhi ambapo kwa sasa bado jitihada za kuwaokoa waliokwama chini zinaendelea na miongoni mwa waliopo kwenye kazi hiyo mbali na Jeshi la Polisi, Zimamoto pia bondia Hassan Mwakinyo ni miongoni mwao huku Asemahle Wallen ambaye naye ni bondia alitarajiwa kuungana nao leo.

Kumbilamoto amesema kuwa anaungana na Rais Samia kuwapa pole wafiwa wote na huku kwa upande wa majeruhi hao wanaombewa dua warejee kwenye afya njema.

“Mungu awape subra katika kipindi hiki kigumu wanachopitia Mungu awasamehe makosa yao Marehenu wetu Amin.”