MSUVA AIKARIBIA REKODI YA NGASSA

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa, Taifa Stars, Simon Msuva katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ethiopia, kumemfanya nyota huyo kufikisha mabao 23 na kuifukuzia rekodi iliyowekwa na Mrisho Ngassa mwenye 25.

Nyota huyo amefunga mabao 23 katika michezo 93 ya timu ya taifa tangu alipokitumikia kikosi hicho rasmi mwaka 2012, huku akibakisha mawili tu kuifikia rekodi ya Ngassa aliyefunga 25, kwenye mechi 100 alizochezea kuanzia mwaka 2006 hadi 2015.

Huku Mbwana Samatta ndiye anayefuatia kwa ufungaji bora wa timu ya taifa baada ya kufunga mabao 22 katika michezo 82, tangu alipoanza kuichezea mwaka 2011, akifuatiwa na nyota, John Bocco mwenye 16, katika michezo 84, aliyocheza kuanzia 2009.