MASWALI ya kujiuliza Yanga kuhama Azam Complex ambpo taarifa rasmi kutoka Yanga ilitolewa Novemba 9 2024 kwa umma kwamba Yanga itautumia Uwanja wa KMC Complex kwa mechi za nyumbani.
Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 Yanga ilikuwa ikiutumia Uwanja wa Azam Complex kwenye mechi za nyumbani na ilikuwa ikipata matokeo msimu wa 2024/25 ni mechi mbili mfululizo imepoteza.
Legend kwenye masuala ya michezo Bongo kitaifa na kimataifa, Saleh Ally, maarufu kwa jina la Jembe ameweka wazi kuwa kuna maswali mengi ya kujiuliza kuhusu Yanga kuondoka Uwanja wa Azam Complex na kuibukia KMC Complex.
Miongoni mwa maswali hayo ni:- Yanga wamehama Azam Complex ila kuna maswali mengi yapo kuhusu suala hilo, je ni Azam Complex imekuwa ikiwazuia Yanga kutengeneza nafasi?
Ni Azam Complex imekuwa ikiwaongoza Yanga kukosa penalti? Kumbuka kwamba kwenye mchezo dhidi ya Tabora United, Aziz Ki alikosa penalti dakika ya 45.
Je ni Azam Complex ni sababu Yanga kufungwa mechi mbili mfululizo? Yanga imefungwa mechi mbili ilikuwa Yanga 0-1 Azam FC na Yanga 1-3 Tabora United?
Je ni Azam Complex inawafanya wachezaji washindwe kufunga?
Wamehamia KMC Complex hapo wakifungwa je tutasema nani amesababisha? Itakuwa Simba ama uwanja?
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.