YANGA NA KIMATAIFA HESABU ZIPO HIVI

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga la kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga wameanza kupiga hesabu kimataifa kuelekea mchezo wao ujao dhidi ya Al Hilal ya Sudan unaotarajiwa kuchezwa Novemba 26 2024.

Yanga chini ya Kocha Mkuu, Sead Ramovic tayari wameanza maandalizi kuelekea mchezo huo wa hatua ya makundi ndani ya msimu wa 2024/25.

Bakari Mwamnyeto nahodha wa Yanga ambaye ni beki chaguo la kwanza la Gamondi ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kwenye mechi zote ambazo wanacheza kitaifa na kimataifa.

“Ambacho tunakifanya ni maandalizi mazuri kwenye kila mchezo kitaifa na kimataifa na tunatambua kwamba hakuna ambaye hapendi kuona tukipata matokeo mazuri uwanjani.

“Benchi la ufundi linatupa mbinu ambazo tunazifuata ili kuzifanyia kazi uwanjani, makosa yaliyopita hayo yanafanyiwa kazi kwenye uwanja wa mazoezi kwa kuwa malengo ni kuona tunakuwa imara na kupata ushindi kitaifa na kimataifa.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.