KIKOSI cha Simba chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids ni wakali wa kufunga mabao mengi ndani ya 18 katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2024/25 ambao una ushindani mkubwa mwanzo mwisho.
Ndani ya NBC Premier League ni mabao 19 mastaa wa Simba wamefunga ikiwa ni namba moja katika timu zilizofunga mabao mengi ndani ya 18.
Kwa sasa burudani za ligi zimesimama kwa muda kutokana na timu za taifa kuwa na kazi kimataifa ambapo Tanzania ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ethiopia kwenye mchezo wa kuwania kufuzu AFCON 2025 mabao yakifungwa na Simon Msuva dakika ya 15 na Feisal Salum dakika ya 30 ilikuwa ni Novemba 16 2024.
Wakati Simba wakiwa ni namba moja kwenye wakali wa kutupia na kinara akiwa ni Jean Ahoua mwenye mabao matano Fountain Gate ni namba mbili ikiwa imetupia mabao 14 inafuatiwa na Azam FC ambayo imetupia mabao 12.
Tabora United ni mabao 10 huku Yanga inayonolewa na Kocha Mku Sead Ramovic ikiwa imetupia mabao 9.