ALI Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa kupoteza mchezo wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara kumewapa maumivu kwa kuwa wamesemwa mpaka na mama.
Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 Yanga ilicheza mechi 8 haikupoteza ilishinda kwenye mechi zilizo ndani ya tatu bora kwa kuifunga Simba 0-1 Yanga, Singida Black Stars 0-1 Yanga.
Ni Novemba 2 2024 ubao wa Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90 ubao ukasoma Yanga 0-1 Azam FC mtupiaji akiwa ni Sillah dakika ya 33 kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Mara baada ya Yanga kupoteza Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alituma ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kwa kuandika namna: “Hongereni Azam kwa ushindi dhidi ya Yanga katika mchezo wenu wa Ligi Kuu.
Pamoja na Klabu nyingine zinazoshiriki Ligi Kuu, mnaendelea kutupa Watanzania burudani kupitia soka huku Taifa likiendelea kuchapa kazi kwa amani, umoja na utulivu. Nawatakia kila la kheri.
Kamwe akaandika namna hii: “Leo tumesimangwa hadi na Mama, imeniuma sana.”