MOHAMED Hussen Zimbwe Jr, beki wa kazi ndani ya kikosi cha Simba amefichua siri nzito ambayo inampa nguvu ya kudumu kwenye ubora wake uleule muda wote akiwa uwanjani katika mechi za ushindani.
Ipo wazi kuwa wamepita makocha wengi ndani ya kikosi cha Simba hivi karibuni ikiwa ni Patrick Aussems ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Singida Black Stars, Didier Gomes, Roberto Oliveira, Thiery Hitimana lakini Zimbwe alikuwa chaguo la kwanza.
Kwa sasa Simba inanolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids beki huyo ambaye ni nahodha bado ni chaguo la kwanza na mchezo dhidi ya Namungo alianzia benchi aliingia dakika ya 75 kuchukua nafasi ya Nouma.
Zimbwe amesema kuwa siri kubwa ya kudumu kwenye ubora huo ni Mungu pamoja na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi jambo ambalo linamfanya adumu kwenye ubora huo kila wakati.
“Kikubwa ni Mungu kwa kuwa namtanguliza yeye kila wakati bila kusahau kufuata maelekezo ya benchi la ufundi kwani wao wananipa maelekezo ambayo ninayafuata nikiwa uwanjani.
“Ushirikiano uliopo kwenye timu unatupa matokeo mazuri na ambacho tunahitaji kuwa kwenye mwendelezo bora muda wote inawezekana,mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwani wao wanatuongezea nguvu ya kupambana zaidi.”
Novemba Mosi 2024 wakati ubao wa Uwanja wa Lake Tanganyika ukisoma Mashujaa 0-1 Simba, Zimbwe alianza kikosi cha kwanza.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.