ILIKUWA ni vita yenye mwendelezo wa msako wa pointi tatu ndani ya uwanja ambapo kila timu ilipambana kuonyesha ubora wake dakika 90 mwanzo mwisho licha ya ushindi bado haijaisha kwa kuwa kuna mzunguko wa pili unakuja.
Simba imekuwa na kawaida ya kutumia dakika 15 za kipindi cha kwanza kupambana kusaka bao la mapema kisha dakika zinazofuata hucheza kwa hesabu tofauti kabisa.
Kumbuka kwamba kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons baada ya kupata bao la mapema dakika ya 5 kupitia kwa Che Malone mpango kazi ulibadilika na ilikuwa hivyo dhidi ya Namungo Uwanja wa KMC, Mwenge.
Ndani ya dakika 5 walipata bao la mapema kupitia kwa Shomari Kapombe na wakapata bao lingine kupitia kwa Jean Ahoua dakika ya 33, kamba ya tatu ilifungwa na Mavambo dakika ya 84.
Namungo walikuwa wakicheza kwa kujilinda na moja ya jaribio walifanya kipindi cha kwanza kupitia kwa Hassan Kabunda na mlinda mlango Camara alifanikiwa kuliokoa.
Kuingia kwa Meddie Kagere kuliongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji licha ya kwamba zaidi ya mara mbili Kagere alikutwa kwenye mtego wa kuotea.
Leonel Ateba amekuwa kwenye mwendo wa tofauti kwenye mechi mbili mfululizo anatengeneza nafasi katoa pasi yake ya kwanza ndani ya ligi akimpa Mavambo na Mukwala amekuwa imara kwa kufanya majaribio na pasi yake ya kwanza alimpa Ahoua.
Shomari Kapombe mchezaji bora wa mchezo Oktoba 25 2024 lakini alipoteza pasi nyingi akiwa ndani ya 18 katika matukio muhimu anapaswa kuimarika kuwa bora zaidi.
Simba inafikisha pointi 19 baada ya kucheza mechi 8 nafasi ya pili kwenye msimamo vinara ni Singida Blacks Stars ambao Oktoba 25 2024 waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate ya Issa Lipoda.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.