WALICHOFANYA MASTAA WA SIMBA NA TANZANIA PRISONS

MASTAA wa Tanzania Prisons na Simba walikuwa na kazi ya kusaka pointi tatu muhimu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, Oktoba 22 Uwanja wa Sokoine baada ya dakika 90 ubao ukasoma Tanzania Prisons 0-1 Simba. Kila nyota alifanya kazi kubwa kutimiza majukumu yake na hapa tunakuletea baadhi ya walichofanya mastaa wa timu hizo namna hii:-

MOUSSA CAMARA

Kipa wa Simba alianza kikosi cha kwanza aliokoa hatari dakika ya 53, 54, 59, 82 alipiga faulo dakika ya 74. Alikomba dakika 90 na hakufungwa.

CHE MALONE

Alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo, alifunga bao dakika ya 5 akiwa ndani ya 18, alicheza faulo dakika ya 29, aliokoa hatari dakika ya 85.

AWESU AWESU

Alipewa jukumu la kupiga faulo dakika ya 46, alipiga kona dakika ya 51 alichezewa faulo dakika ya 27, 28, alipiga krosi dakika ya 41 na alikomba dakika 61 nafasi yake ilichukuliwa na Joshua Mutale ambaye alipiga kona dakika ya 76, 78, alichezewa faulo dakika ya 77, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 62.

LADACK CHASAMBI

Alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 63, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 28, alikomba dakika 84 nafasi yake ilichukuliwa na Mzamiru Yassin.

KIBU DENNIS

Alipiga faulo dakika ya 5, 38, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 31, alichezewa faulo dakika ya 60, 74.

MOHAMED HUSSEN

Alipiga faulo dakika ya 35, alichezewa faulo dakika ya 38, alipewa majukumu ya kurusha dakika ya 39, 49 alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 40. Alikomba dakika 61 nafasi yake ilichukuliwa na Edwin Balua ambaye alipiga faulo dakika ya 73, 77.

SHOMARI KAPOMBE

Aliokoa hatari dakika ya 36 alipewa majukumu ya kurusha dakika ya 45, 90 alipiga faulo dakika ya 67.

LEONEL ATEBA

Alichezewa faulo dakika ya 28, alipiga krosi dakika ya 52, 63, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 69 shuti ambalo lililenga lango dakika ya 58. Alikomba dakika 72 nafasi yake ilichukuliwa na Steven Mukwala aliyepiga mashuti yaliyolenga lango dakika ya 76, 85.

CHA MOAH

Alichezewa faulo dakika ya 7 aliokoa hatari dakika ya 45, 88 alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 47.

HAWA HAPA MASTAA WA TANZANIA PRISONS

MUSSA MBISA

Kipa namba moja wa Tanzania Prisons alianza langoni kutimiza majukumu yake, dakika ya 5 alitunguliwa bao moja na Che Malone kwa kosa la kutema mpira uliopigwa na Kibu Dennis.

Aliokoa hatari dakika ya 37, 41, 55, 56, 64, 73, 76. Alikomba dakika 90 kwenye mchezo huo wakiwa nyumbani.

HAJI MUSSA

Anaingia kwenye orodha ya nyota walioonyeshwa kadi ya njano ilikuwa dakika ya 27.

HARUNA CHANONGO

Alipiga krosi dakika ya 53 alichezewa faulo dakika ya 29 alikomba dakika 67 nafasi yake ilichukuliwa na Jumanne Elifadhili.

EZEKIEL MWASHILINDI

Alicheza faulo dakika ya 38, 77 alipewa jukumu la kupiga faulo dakika ya 35.

JEREMIA JUMA

Alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 36, alipiga krosi dakika ya 54, alikomba dakika 67.

ISMAIL MHESA

Aliokoa hatari dakika ya 43, 50, 56 alicheza faulo dakika ya 40, 74 alionyeshwa kadi ya njano.

SAMSON MBANGULA

Nyota huyu alianza kikosi cha kwanza alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 42.

ZABONA MWAYOMBWA

Aliokoa hatari dakika ya 43, alipiga krosi dakika ya 55 alikomba dakika 82.

DOTTO SHABAN

Alipiga shuti ambalo halikulenga lango ilikuwa dakika ya 86 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 75.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.