MAKIPA BONGO MAKOSA YAO YANAWAADHIBU

KWENYE mechi mbili mfululizo, Mussa Mbisa kipa namba moja wa Tanzania Prisons amefanya kosa moja lililoigharimu timu kufungwa bao moja.

Rekodi zinaonyesha kuwa mchezo dhidi ya Azam FC Uwanja wa Sokoine alifungwa bao moja kwa kosa la kutema mpira mtupiaji alikuwa Idd Nado dakika ya 11 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Sokoine ulisoma Prisons 0-2 Azam FC.

Mchezo wa pili ilikuwa dhidi ya Simba alifanya kosa linalofanana akafungwa bao moja na Che Malone ilikuwa dakika ya 5 kutokana na kosa la kutema mpira uliopigwa na Kibu Dennis.

Kumbuka kwamba Sio Mussa Mbisa mwenye makosa hayo hata kipa wa Simba Moussa Camara naye makosa hayo anayo alifanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya Yanga, zaidi ya mara mbili akafungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 86.

Mwingine ni kipa wa Coastal Union, Ley Matampi, Oktoba 4 2024 wakati ubao wa Uwanja wa KMC ukisoma Simba 2-2 Coastal Union alifungwa bao moja na Mohamed Hussen baada ya mpira kumponyoka mkononi.

Makipa wa Bongo wanakazi kubwa kuboresha makosa yao ili kuwa bora zaidi kwenye mechi za ushindani kitaifa na kimataifa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.