MUSSA CAMARA KWENYE MTEGO MZITO

KIPA namba moja wa Simba, Mussa Camara yupo kwenye mtego mzito kurejesha hali ya kujiamini katika kikosi cha kwanza kutokana na mwendo ambao amekuwa nao kwa sasa.

Ikumbukwe kwamba kipa huyo kwenye mechi nne mfululizo ambazo alianza kikosi cha kwanza katika mechi za Ligi Kuu Bara hakufungwa na alikuwa imara kwenye kucheza na kutoa maelekezo kwa wachezaji wenzake ndani ya uwanja.

Baada ya kufungwa kwenye mchezo wa tano dhidi ya Coastal Union kutokana na makosa ya kutoka kwenye eneo lake na washambuliaji kusoma tabia hiyo ghafla ameanza kuonekana kupoteza hali yake hiyo ya kujiamini licha ya kufanya kazi kubwa kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi, Oktoba 19 2024.

Wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 0-1 Yanga, Camara katika harakati za kuokoa alitema mpira uliokuwa mikooni mwake na kuuludisha ndani ya 18 jambo lililompa nafasi Maxi Nzengeli kufunga bao dakika za lala salama.Ikumbukwe kuwa haikuwa mara ya kwanza kufanya kosa kama hilo hivyo anajukumu la kuongeza umakini katika kutimiza majukumu yake.

Ni mechi sita ambazo Simba imecheza dakika 540, kipa huyo kafungwa mabao matatu kwenye mechi mbili mfululizo ambazo ni dakika 180. Oktoba 22 2024 Simba ina kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Tanzania Prisons mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

HIZI HAPA MECHI ZA CAMARA

Simba 3-0 Tabora United mchezo huu ulichezwa Uwanja wa KMC, Mwenge ilikuwa Agosti 18 2024 ni mchezo wa kwanza kwa Simba kwenye ligi na mtupiaji bao la kwanza ni Che Malone ilikuwa dakika ya 14 akitumia pasi ya Jean Ahoua.

Simba 4-0 Fountain Gate, huu ulikuwa ni mchezo wa pili kwa Simba ulichezwa Uwanja wa KMC, Mwenge ilikuwa Agosti 25 2024.

Azam FC 0-2 Simba huu ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Simba kucheza ugenini ulichezwa Uwanja wa New Amaan Complex Septemba 26 2024.

Dodoma Jiji 0-1 Simba ilikuwa Septemba 29 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma walisepa na pointi tatu kwenye mchezo huu.

Simba 2-2 Coastal Union uliochezwa Uwanja wa KMC, Mwenge ilikuwa ni Oktoba 4 2024.

Oktoba 14 2024, Simba 0-1 Yanga mchezo wa kwanza kupoteza mtupiaji ni Maxi Nzengeli dakika ya 86.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.