DROO ya Kombe la Shirikisho imepangwa nchini Misri ambapo wawakilishi kwenye anga hilo kutoka Tanzania ni Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.
Simba imepangwa kundi A na ilikuwa POT 1 lililokuwa na Zamalek, RS Berkane, Simba, USM Alger ambazo hizi hazitakuwa pamoja kwenye makundi na POT 2 lilikuwa na ASEC Mimosas, Stade Malien, Al Masry na CS Sfaxine, POT 3 lilikuwa na Enyimba, ASC Jaraaf ambazo hizi hazitakutana.
Makundi yapo namna hii:-
KUNDI A
Simba
CS Sfaxien
CS Constantine
FC Bravos do Maquis
KUNDI B
RS Berkane
Stade Malien
Stellenbosch
CD Luanda
KUNDI C
USM Alger
ASEC Mimosas
ASC Jaraaf
Orapa United
KUNDI D
Zamalek SC
Al Masry
Enyimba FC
Black Bulls