>

MAXI NZENGELI BALAA ZITO

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga Maxi Nzengeli ana balaa zito uwanjani kutokana na kuwa na uwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi za mabao kwenye mechi za ushindani msimu wa 2024/25 akiwa namba moja kwa wakali wa kutupia ndani ya Yanga kwenye ligi.

Ni mabao matatu anayo kibindoni akiwa amefunga mabao hayo ugenini bao moja na Uwanja wa Azam Complex amefunga mabao mawili na ipo wazi kwamba yeye ni mchezaji wa kwanza ndani ya kikosi cha Yanga kufunga msimu wa 2024/25.

Sio kwenye ligi tu bali alianza mwanzo wa msimu ambapo alifunga kwenye Kariakoo Dabi mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa Uwanja wa Mkapa ilikuwa Agosti 8 2024 dakika ya 44 bao hilo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo

Kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC  fainali Agosti 11 alitoa pasi mbili zilizoleta mabao ilikuwa dakika ya 30 kwa Aziz Ki na 27 kwa Boka

Ukiweka kando katika Ngao ya Jamii ambayo ipo mikononi mwa Yanga alifunga bao la kwanza mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba na bao la pili kwenye ligi alifunga dakika ya 4 mbele ya KMC Uwanja wa Azam Complex ilikuwa Septemba 29 2024 bao la ushindi

Alifunga bao la tatu mbele ya Pamba Jiji Uwanja wa Azam  Complex ilikuwa Oktoba 3 dakika ya 54 alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo. Kituo kinachofuata ni dhidi ya Simba mchezo wa Kariakoo Dabi Oktoba 19 Uwanja wa Mkapa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Myuka, Mtunzi Kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kuipata 0756 028 371